Nyimbo za wokovu (n°40)
1. Ameniweka huru kweli, naimba sasa: Haleluya!
Kwa musalaba nimepata, kutoka katika utumwa.
Refrai:
Nimeokoka nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka.
Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.
2. Zamani nilifungwa sana, kwa minyororo ya Shetani,
nikamwendea Bwana Yesu, akaniweka huru kweli.
3. Neema kubwa, nilipata kuaca njia ya mauti.
Na nguvu ya wokovu huo, yanichukuasiku zote.
4. Na siku moja nitafika, mbinguni kwake Mungu wangu.
Milele nitamhimidi, na kumwimbia kwa shukrani.